Wanawake.
Wakati ndio huu, ngoja nikuelezee.
1.Hata kama ukiwa ni Rais, ukiwa maarufu , ukiwa ni mfanyabiashara mkubwa kiasi gani. Hivi vitu vinabaki Ofisini kwako, shuleni kwako, kanisani kwako,gym kwako, Uzuri zaidi kila mahali kuna wanawake.
Lakini Kulaumu na kunyoshea vidole sio kitu kizuri, huwezi kutatua tatizo. Habari mpya haitatui kitu. sana sana inaleta fujo na kelele na kuingiza woga. hivyo ni vitu vya kufanya nyuma ya pazia lakini hakuna kinachofanyika.
Mwanamke anapoamua kuongeza mwili kwa ajili ya kujipenda mwenyewe na kufurahia jinsi alivyo, Ni tatizo
Mwanamke anapopungua mwili ili kujifurahisha mwenyewe pia ni tatizo
Anapovaa nguo kwa ajili ya nafsi yake, afurahie mwenyewe , ni tatizo
Mwanamke anapokuwa amebakwa katika maisha yake, kufanyisha kitendo bila ridhaa yake ni tatizo.
Ni tabia. Ni tabia ya wanaume ndio inayoathiri kiasi kikubwa cha tabia za wanawake.
2.Tabia hizi zimefanya wanawake wengi waamini kitu ambacho sio sahihi. tabia hizi zimeharibu imani zao. Ulimwengu na wanaume wamesababisha. Na jinsi gani imani hizo zimeingia katika mahusiano na katika mapenzi.
Mwanamke kufanya sex bila ya ridhaa yake, kusimangwa, kudharauliwa. Ni kitu cha nguvu. Unapomsema mtu au kumdharau mtu , unaondoa kitu ndani yake, sauti zao, uhuru wao, heshima zao, nguvu zao.
Vitu hivi vinapotokea wakati wa umri mdogo, vinakomaa, vinafunga watu, na kujikuta wanaishi au kulala na adui. kwa sababu inaonekana kama kitu cha kawaida. Kwa sababu ya kupotesa thamani, kujiona hustahili. unaweza kuvutiwa hata na mtu ambaye anakuumiza. unataka kuhakikishwa na wao na kuboreshwa na wao. Makosa ambayo unafanya ni katika sex. Na sasa unakuwepo kwenye mahusiano yenye sumu mbaya. Hapo unakosa maono yako na kukutana na afya mbaya katika maisha yako yote. Unakosa Upendo wa kweli. Unakosa maana ya maisha.
Kwa mtindo huo mwanamke atakuwa anahisi kukosa usalama, anajiona sio kitu, atakuwa mwoga, anaona aibu na kujiona kuwa na hatia. Badala ya Upendo ataishi na mwanaume kwa mazoea bila ya upendo wa kweli.
Hii ni sumu ambayo inaingia kwenye mishipa kama vile kuchomwa sindano bila ya kupenda.
3.Hiki kinakuwa ni kirusi ambacho kimekula ustahili wake. Anakuwa mtu wa kupigana na kukimbia, haijalishi ni jambo kubwa la aina gani lakini tayari anakuwa yupo kwenye kifungo. Atakuwa hawezi kujielezea, kujiwekea mipaka, kujenga usalama wake. atapata shida ya kuamini mtu, shida ya mwili, shida ya kula , huzuni na mengine.
4.Mwanaume.
Ni wakati wa kuangalia.Kwa sababu hili sio tatizo la mwanamke.Hili ni tatizo la watu linaathiri mahusiano. Linaathiri mabinti zetu. Inakuathiri wewe na mahusiano yako
Kwa hio mtu ambaye unaishi naye, ni mama wa watoto wako. Ni rafiki yako, Ni soulmate wako, ni mwili wako. Mpende kama unavyopenda nafsi yako.
Hii haihusu wanaume wengine . Inakuhusu wewe. Mchango wako ni upi katika Ulimwengu huu. Unamfikiaje mwanaume mwenzako na kumpa Elimu ya kuishi ipasavyo na mwanamke aliyenaye?
Kuwa mwanaume bora sio kujiamini mwenyewe, sio kuwa na heshima yako, sio jinsi unavyotambulika na watu. Ni Katika matendo yako ya kiume .Kuwa mwanaume sio sex. Kuwa mwanaume ni Kuwa na Akili iliopevuka, akili ya kusaidia wengine wajielewe. Hakuna kitakachobadilika kama hakuna badiliko.
Inawezekana hujawahi kubaka, lakini wapo wanaobaka bila ya kujua, wanafikiri ni sahihi. Huenda hujawalaumu wanawake lakini wapo wanaodharau na kulaumu wanawake katika mambo mengi. Elimisha mwanaume mmoja atamwelimisha na mwingine.
Jaribu kujichunguza ulipo sasa. Nguvu gani unayoweka ndani ya mahusiano yako? Nia yako, maneno yako na matendo yako yakoje?
Mawasiliano yako ni mazuri? Unao muda wa kumsikiliza mke wako? Unamwambia ukweli anapokuwa amekosea? Kusikiliza ni zaidi ya maneno . Unamkubali jinsi alivyo?
Ni rahisi kujificha nyuma ya simu katika mawasiliano. Kitu kinachokuunganisha ndicho kinakutenga. Unajipoteza mwenyewe, unafunga moyo wako mwenyewe. Unapokuwa huwasiliani uso kwa uso, unamweka mtu gizani na kuleta hali ya kukosa usalama. Wasiliana na mke wako kwa kuongea naye karibu, uwe wazi. hata kama ni mazingira magumu. Mwanaume hujionyesha.
Haijalishi umempata mwanamke mwenye historia ya aina gani, huenda ameolewa mara kumi, alikuwa malaya, au mwizi, rafiki. ukimpenda mwonyeshe thamani yake ya uanamke. Ili ajisikie kuwa yuko salama.

No comments