Tofauti Kati Ya Almost Relationship Na Serious Relationship

Tofauti Kati Ya Almost Relationship Na Serious Relationship

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, Kamwe hutaweza kuongea kuhusu maisha ya baadae.Unakuwa unaepuka mipango yote inayohusu baadae. Unaweza kuwa unafanya kila kitu lakini  hutaweza kuongea kuhusu baadae.

Lakini kama upo kwenye serious relationship, Topic yako muda wote itakuwa kuhusu baadae. Utaongea kuhusu mipango yote ya baadae,  Aina gani ya nyumba, Watoto wangapi,  Marafiki wa aina gani, Harusi itakuwaje,  Utaongea jinsi gani mtakavyoweza kukua pamoja.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida , Utakuwa unaficha hisia zako. Unacheza na ukweli.  unakuwa unaonyesha kujali kidogo sana kuliko uwezo wako, kwa sababu sio mahali pa kudumu. Hautaki kuwa na nguvu kubwa hapo, kwa hio unakuwa unapretend.

Lakini kama upo kwenye  mahusiao ya kweli, utaonyesha hisia zako bila ya kuficha .Utamwambia mtu huyo anapokuwa anavutia na kushangaza.  Utamwambia unapotaka akukumbatie, akukiss, utamwambia jinsi gani unampenda. Utamfanyia anachostahili. Huwezi kuficha upendo ulionao kwake.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, unapima kila kitu mtu anapokuwa anafanya , hata kama ni kidogo.  Hata kama atatuma ujumbe ambao hujaelewa, utaanza kulalamika, kila kitu unakichukulia tofauti, huna majibu . hata kama utaongea naye huwezi kujisikia vizuri.

Lakini unapokuwa kwenye serious relationship, utasema unachokimaanisha na kutegemea upande wa pili kusema vile vile.kama akikutumia ujumbe usioeleweka, utajiuliza ana maana gani. hautakuwa na shaka.  utapata majibu sahihi, na mtaongea pamoja.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, unakuwa huelewi maana ya kuwa na huyo mtu.Kwa hio hutaweza kujua mipaka yake.  Hutaweza kumwonyesha kwa watu, hutaweza kumpeleka nyumbani kwenu, hutaweza kukaa nae kwa muda mrefu usiku,Kwa sababu huna uhakika.

Lakini unapokuwa kwenye mahusiano ya kweli, unafahamu mipaka ya mwingine, na pia mipaka yako inakuwepo vizuri.  utafahamu kitu gani wanakipenda na kipi hawakipendi.  Utafahamu kabisa kuwa kuna kitu anatarajia kwako.  unafahamu kabisa kuwa unahitaji kupata kitu cha  furaha kutoka kwako.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida,  mara zote utakuwa huelewi. Maswali ya haraka, kutokuwa na uhakika  wa hisia zako na hisia za mwingine, huna uhakika kama utaweza kuwa pamoja.  huna uhakika kwa kila nguvu unayotumia kwa mtu huyo.

Lakini kama upo kwenye mahusiano ya kweli, Huna muda wa kuwa na shaka. Unajisikia vizuri kila unapokuwa naye.Kama vile ni mahali hasa ambapo ulitakiwa uwepo. Ni kama umefika nyumbani kwako.Mahali pa usalama.

No comments